Simba Sports Club
News

TAARIFA KWA UMMA.

7 Nov 2023 By simbasc 309 views
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo ( Robetinho). Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana. Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya. Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola. Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde. Simba Nguvu Moja. Imani J. Kajula Afisa Mtendaji Mkuu Simba Sports Club 07 Novemba 2023
Advertisement
Back to homepage
Share this story