Simba Sports Club
News

Steve Barker ndiye kocha wetu Mkuu

19 Dec 2025

Barker (57) raia wa Afrika Kusini amejiunga na kikosi chetu akitokea Stellenbosch FC ya nchini Afrika Kusini.

Kocha Barker ana leseni A ya Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA pamoja na Leseni A ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF)

Barker anachukua nafasi ya Meneja Mkuu Dimitar Pantev raia wa Bulgaria ambaye mkataba wake ulivunjwa mwezi uliopita kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu.

Advertisement

Mbali na kuifundisha Stellenbosch pia amewahi kuzinoa timu za Black Aces FC, AmaZulu FC na U. Pretoria zote za nchini Afrika Kusini.

Msimu wa 2023/24 aliiwezesha Stellenbosch kufika nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Msimu wa 2023/2024 aliiwezesha Stellenbosch kutwaa ubingwa wa Carling Knockout Cup.

Barker atakuja na wasaidizi wake wanne na muda wowote kutoka sasa atawasili nchini.

Back to homepage
Share this story