Simba Sports Club
News

Stars yaanza kwa ushindi CHAN

2 Aug 2025

Stars iianza mchezo huo kwa kasi huku ikifika zaidi langoni mwa Burkina Faso lakini ikikosa utulivu wa kutumia nafasi ilizotengeneza.

Abdul Suleiman Sopu alitupatia bao la kwanza dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya mshambuliaji Clement Mzize kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kipindi cha pili Stars ilirudi kwa kasi zaidi ikiongeza umakini na kufanya mashambulizi zaidi lakini kikwazo kikubwa kikiwa kwa mlinda mlango wa Burkina Faso.

Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' aliipatia Stars bao la pili kwa kichwa dakika ya 71 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Idd Suleiman 'Nado'.

Advertisement

Michuano ya CHAN inafanyika katika nchi tatu za Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda.

X1: Yakubu, Kapombe, Zimbwe Jr, Bacca, Job, Kagoma, Nado (Mwaikenda 82'), Mudathir, Mzize, Feisal, Sopu (Msindo 72')

Waliionyeshwa kadi: Mudathir Yahya, Yusuph Kagoma

Back to homepage
Share this story