Simba Sports Club
News

Sita waitwa Stars kujiandaa na CHAN

27 Jun 2025

Taifa Stars itaingia kambini Julai 7 kujiandaa na michuano hiyo ambayo Tanzania ni miongoni mwa nchi mwenyeji.

Mlinda mlango Aishi Manula amerejeshwa kwenye kikosi cha stars baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kufuatia majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.

Advertisement

Nyota wengine walioitwa ni walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' na Abdulrazack Hamza.

Wengine ni kiungo Yusuph Kagoma na kiungo mshambuliaji Kibu Denis.

Back to homepage
Share this story