Katika hafla hiyo ambayo wageni wetu walipata nafasi ya kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu ujio wao na vitu gani watavifanya katika muda wote watakao kuwepo nchini.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Othman Yakub, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayay, Katibu Mtendaii wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha na Msimamizi wa Uwanja wa Mkapa, Gordon Nsajigwa ni miongoni mwa Viongozi wa Serikali waliohudhuria chakula hicho.
Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) liliwakilishwa na Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko, Boniface Wambura na Meneja wa Leseni za klabu, Jonas Kiwia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Muhene, Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu, Mjumbe wa Bodi, Asha Baraka, Mtendaji Mkuu wa klabu, Imani Kajula na baadhi wa wafanyakazi kutoka Menejimenti wamewakilisha klabu katika tukio hilo.