Kikosi chetu kimetua salama nchini Zambia jioni kikiwa tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows Jumapili.
Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez amesema kikosi kilitakiwa kuwasili Zambia mchana lakini kutokana na baadhi ya taratibu za usafiri wa ndege kuchelewa kimetua jioni.
Baada ya kuwasili Zambia kikosi kimepokelewa vizuri na wenyeji Arrows kwa kushirikiana na Chama cha Soka nchini humo na hakukukuwa na changamoto yoyote nje ya uwanja.
"Kikosi kimewasili salama hapa Zambia, wenyeji wetu wametupokea vizuri hatujapata changamoto yoyote mpaka sasa. Tumefika Uwanja wa Ndege tumetumia dakika 15 tu kutoka," amesema Barbara.
Barbara ameongeza kuwa licha ya kikosi kuchelewa kufika lakini Kocha Pablo Franco amesema lazima kifanye mazoezi ya utimamu wa mwili ili kesho kifanye mara ya mwisho tayari kwa Jumapili.