Simba Sports Club
News

Simba yatua Mwanza kuivaa Ruvu Shooting

1 Jun 2021 By simbasc 2,999 views

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Mwanza leo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM  Kirumba Alhamisi Juni 3, mwaka huu.

Timu imeondoka na jumla ya wachezaji 20 ambapo  jioni itafanya mazoezi ya kuweka miili sawa tayari kwa mchezo huo.

Mchezo huo ni wa kiporo ambapo ulisogezwa mbele kutokana na ushiriki wetu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement

Tunaingia kwenye mchezo dhidi ya Ruvu tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo tuliopata Jumamosi iliyopita.

Kuelekea ukingoni mwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2020/21 tumejiandaa kuhakikisha tunashinda mechi zote nane zilizobaki ili kutetea ubingwa wetu kwa mara ya nne mfululizo.

Back to homepage
Share this story