Waziri Simai amechukua uamuzi huo kwa kutambua mchango mkubwa klabu yetu katika kutangaza utalii wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
Klabu ya Simba ilianzisha mkakati wa kuitangaza Zanzibar kupitia kauli mbiu ya Visit Zanzibar katika jezi na mitandao yetu ya kijamii wakati huu wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Advertisement
Akizungumza kwa niaba ya klabu ya Simba Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amsema,“ tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutambua mchango wa timu yetu kutangaza utalii hivyo kukuza uchumi, tunaona fahari kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi.”