Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam leo asubuhi kikitokea Mtwara ambapo wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja.
Baada ya mchezo dhidi ya Namungo juzi kikosi kilirejea Mtwara usiku ule ule na jana jioni kilifanya mazoezi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona kurejesha utimamu wa mwili kwa wachezaji (recovery).
Advertisement
Baada ya mapumziko ya siku moja kesho kikosi kitasafiri kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Juni 3, mwaka huu.
Sisi ndio vinara wa Ligi Kuu tukiwa na alama 64 baada ya kucheza mechi 26 tukiwa na michezo mitatu mkononi.