Simba Sports Club
News

Simba yapokelewa kifalme Kigoma

22 Jul 2021 By simbasc 1,436 views

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Timu ya Simba, imepata mapokezi makubwa baada ya kutua mkoani Kigoma tayari kwa Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Lake Tanganyika.

Simba imetua saa 12 jioni hapa Kigoma na kupokelewa na idadi kubwa ya mashabiki ambao wanaonekana kuwa na imani kubwa na timu yao pendwa.

Mapenzi makubwa yaliyoonyeshwa na mashabiki kwenye mapokezi ya leo yamewafanya wachezaji wetu kujiona wana deni kubwa siku ya Jumapili.

Advertisement

Mchezo dhidi ya Yanga tunajua utakuwa mgumu lakini  tutajipanga kuhakikisha tunawapa furaha Jumapili.

Back to homepage
Share this story