Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona hapa Mtwara ili kuweka miili sawa baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC.
Timu iliwasili Mtwara jana usiku baada ya kutoka Lindi ilipokuwa na mchezo dhidi ya Namungo tulioibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Advertisement
Mazoezi ya leo pia ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba Juni 3, mwaka huu.