Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali imetoka leo ambapo tumepangwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Johannesburg kati ya Aprili 14/15 kabla ya kurudiana jijini Dar es Salaam wiki mbili baadae.
Advertisement
Katika hatua ya makundi tuliibuka kinara wa kundi wa A dhidi ya miamba ya soka Afrika, Al Ahly, El Merrikh na AS Vita.
Kwenye mechi sita za hatua ya makundi tulishinda nne tukatoka sare mechi moja na kupoteza moja na kufanikiwa kukusanya alama 13.