Kikosi chetu kimeondoka Dodoma kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wa jana dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri.
Baada ya kufika Dar es Salaam wachezaji watapewa mapumziko ya siku chache kabla ya kurudi mazoezini.
Wachezaji walioitwa kwenye timu zao za Taifa watakwenda kujiunga na wenzao huku wengine wakiendelea na mapumziko waliyopewa.
Advertisement
Nyota wetu tisa akiwamo Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Israel Patrick, Kennedy Juma, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na John Bocco wameitwa kwenye Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Benin utakaopigwa Oktoba 7 nchini kabla ya kurudiana siku tatu baadaye ugenini