Simba Sports Club
News

Simba yakabidhiwa mamilioni ya Ubingwa 2020/21

21 Oct 2021 By simbasc 747 views

Timu yetu imekabidhiwa Sh milioni 100 baada ya kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Msimu wa 2020/21 katika usiku wa Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) 2021 zinazofanyika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni mgeni rasmi na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu, Salum Abdallah 'Try Again' na Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez.

Advertisement

Pia timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imekabidhiwa kitita cha Sh milioni 15 baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake 'Serengeti Lite Premier League' msimu uliopita.

Back to homepage
Share this story