Simba Sports Club
News

Simba yajipima tena na Cambiaso

11 Oct 2021

Kikosi chetu leo kimecheza mchezo wa kirafiki wa kimazoezi na Timu ya Cambiaso Sports uliofanyika Uwanja wa Boko Veterans na kumalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Siku mbili zilizopita tulicheza mchezo wa kirafiki wa kimazoezi na timu hiyo kwenye uwanja huo huo ukamalizika kwa kuwafunga mabao 4-1.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini umakini wa safu za ushambuliaji zilifanya mabao yasiwe mengi.

Mlinzi wa kati, Henock Inonga alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 19 baada ya kuunganisha mpira wa adhabu wa uliopigwa na Ibrahim Ajib.

Baada ya bao hilo timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku kosa kosa zikiwa nyingi na kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa bao hilo.

Advertisement

Kipindi cha pili Kocha Didier Gomes aliwatoa Ibrahim Ajib, Gadiel Michael, Jonas Mkude, Said Norshad, Ally Salum na Mzamiru Yassin na kuwaingiza Yussuf Mhilu, Saido Kanoute, Shomari Kapombe na Ambokile, Jeremiah Kisubi na Abdul Swamad Kassim.

Cambiaso walisawazisha bao hilo dakika ya 68 kupitia kwa Clement Kabela baada ya walinzi wetu kufanya makosa.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Said Noshard(43), Gadiel Michael (2), Erasto Nyoni(18), Henock Inonga (29), Jonas Mkude(20) Hassan Dilunga (24), Mzamiru Yassin (19) Jimmyson Mwanulke(21), Ibrahim Ajib (10) Bernard Morrison (3).

Back to homepage
Share this story