Simba Sports Club
News

Simba yaingia kambini kujiandaa na Polisi Tanzania

25 Oct 2021 By simbasc 64,355 views

Kikosi chetu kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Jumatano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Baada ya mchezo wa jana timu imeingia moja kwa moja kujiandaa na mechi hiyo ambayo tunahitaji ushindi ili kurejesha imani kwa mashabiki.

Advertisement

Meneja wa Timu Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na maandalizi yanaendelea lengo ni kukahikisha tunapata alama tatu muhimu.

"Timu imeingia kambini tangu jana baada ya mchezo kujiandaa na mechi ya ligi dhidi ya Polisi utakaopigwa Jumatano na maandalizi yanaendelea vizuri," amesema Rweyemamu.

Back to homepage
Share this story