Simba Sports Club
News

Simba yaichakaza Yanga KMC Complex

21 Dec 2025

Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally ndiye alikuwa nahodha wa timu katika kikosi chetu wakati Ally Kamwe akiwaongoza mashabiki wa Yanga.

Mtangazaji wetu Thobias Sebastian alitupatia bao la kwanza dakika ya tatu baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja akiwa nje ya 18.

Mohamed Hamis 'Dkt. Mo' alitupatia bao la pili dakika ya nane baada ya kumzidi ujanja mlinda mlango wa Yanga.

Advertisement

Mchezo huo ambao ulitakiwa kuchezwa kwa dakika 60 yaani 30 kila upande ulishindwa kumalizika kufuatia mashabiki wa Yanga 'kutia mpira kwapani'.

Lakini hata hivyo licha ya mchezo kushindwa kumalizika katika dakika za mwishoni kipindi cha pili lakini muda uliochezwa mechi ilikuwa nzuri huku tukimiliki sehemu kubwa.

Back to homepage
Share this story