Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la JMK na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hata hivyo tulikosa umakini katika umaliziaji.
Ambokisie Mwaipopo alitupatia bao hilo la pekee kwa kichwa dakika ya 41 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa JMK.
Advertisement
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kushambulia huku tukitengeneza nafasi nyingi ambazo hazikuweza kubadili ubao wa matokeo.
Kabla ya kufungwa na Azam katika mchezo wa nusu fainali kikosi chetu kilikuwa kimeshinda mechi zote nne katika hatua ya makundi.