Mgunda amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri ingawa hali ya hewa ni baridi tofauti na jijini Dar es Salaam.
Mgunda ameongeza kuwa sababu ya timu kuondoka mapema siku tatu kabla ya kucheza mechi ni kuwafanya wachezaji kuzoea hali ya hewa ambayo ni tofauti na nyumbani.
Advertisement
"Tumefika salama Ethiopia, wachezaji wangu wapo kwenye hali nzuri ingawa hali ya hewa ni baridi."
"Tumekuja siku tatu kabla ya kucheza mchezo wetu wa kwanza kwakuwa tunahitaji wachezaji kuzoea hali ya hewa ambayo ni tofauti na nyumbani," amesema Mgunda.