Winfrida, 28 ambaye ni raia wa Kenya amejiunga na Simba Queens kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Fountain Gate Princess.
Winfrida ni mlinda mlango mwenye uwezo mkubwa katika michuano ya ndani na kimataifa ndio maana tumeona atakuwa msaada mkubwa kwa timu.
Advertisement
Winfrida anakuja kuungana na walinda milango wengine mahiri Janeth Shija na Gelwa Yonah na kulifanya lango letu kuzidi kuwa imara.
Usajili wa Winfrida ni pendekezo la kocha Yussif Basigi kuelekea mzunguko wa pili wa ligi lengo likiwa ni kutetea ubingwa wetu.