Wakati zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imesajili wachezaji wawili ili kuongeza nguvu kikosini.
Nyota hao ni mshambuliaji Tagoe Amorkor Mercy raia wa Ghana ambaye alikuwa anacheza katika timu ya Lady Strikers FC.
Mwingine ni Mtanzania, Amina Ramadhani Hemed kutoka Tiger Queens ya Arusha ambaye anaweza kucheza winga zote mbili.
Advertisement
Wachezaji wote wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja kukitumikia kikosi chetu ambacho kasi yake msimu huu si ya kawaida.
Ingawa tuna kikosi chetu ni imara na hatujapoteza mechi wala kutoka sare hafi sasa lakini tunakiboresha kujihakikishia ubingwa tena kwa mara ya tatu.