Simba Queens imeondoka na kikosi kamili cha wachezaji 24 tuliowasajili kwa ajili ya msimu wa mashindano 2024/25 chini ya Kocha Juma Mgunda.
Kikosi kimeondoka huku wachezaji wakiwa na morali ya kwenda kufanya vizuri ili kutwaa ubingwa huo ambao utatupa tiketi ya kuiwakilisha CECAFA kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika.
Advertisement
Kikosi kitafika Ethiopia siku mbili kabla ya kuanza michuano ili kuwapa wachezaji muda wa kuzoea mazingira na hali ya hewa.
Mchezo wetu wa kwanza utakuwa dhidi ya FAD kutoka Djibouti siku ya Jumapili.