Simba Sports Club
News

Simba Queens yamaliza nafasi ya pili TWPL

20 May 2025

Licha ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Bunda Queens lakini haukutosha kutuwezesha kupata ubingwa tukiwa tumelingana pointi na Mabingwa JKT Queens na alama 43 lakini tofauti ya mabao ikiwa kubwa.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa mkali na wakuvutia muda wote mabao yetu yalifungwa na Jentrix Shikangwa na Shelda Boniface.

Advertisement

Shikangwa alifunga bao hilo dakika ya 35 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Aisha Mnuka wakati Shelda alitupia bao la pili mwishoni mwa kipindi cha pili akimalizia mpira Janeth Nyagali.

Kocha Mkuu wa Simba Queens Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Shikangwa na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Asha Djafar na Shelda.

Back to homepage
Share this story