Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukiliandama lango la Tausi tukionyesha dhamira ya kutafuta mabao mengi zaidi.
Mshambuliaji Aisha Mnunka alitupatia mabao mawili ya haraka haraka kabla ya Jentrix Shikangwa kuongeza jingine ambalo lilitufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa 3-0.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi pia ambapo tuliendelea kutengeneza nafasi za kufunga huku Tausi wakijaribu kutushambulia mara kadhaa ingawa matokeo hayakubadilika.
Advertisement
Kocha Mussa Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Elizabeth Wambui, Fasila Odhiambi na Vivian Corazone na kuwaingiza Fatuma Issa, Zawadi Usanase na Cordelia Amarachi.
Matokeo haya yanaifanya Simba Queens kufikisha alama 22 ikiwa kileleni mwa msimamo wa WPL baada ya kucheza mechi nane.