Simba Sports Club
News

Simba Queens yaishushia kipigo kizito Alliance Girls

31 Dec 2024

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo ilituchukua dakika nane kupata bao la kwanza lililofungwa na Elizabeth Wambui kwa shuti kali nje ya 18.

Mshambuliaji Jentrix Shikangwa alitupatia bao la pili dakika ya 23 kwa shuti kali la chini chini baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Alliance.

Dakika 10 baadae Esther Mayala alitufungia bao la tatu baada ya kumalizia Mpira wa adhabu uliopigwa na Precious Christopher na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi ambapo mpira wa mrefu uliopigwa na mlinda mlango Janeth Shija ulimfikia Jentrix ambaye aliwazidi maarifa walinzi wa Alliance na kutufungia bao safi la nne dakika ya 57.

Advertisement

Precious Christopher alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tano dakika ya 80 na kutuhakikishia alama tatu muhimu ugenini.

Kocha Mkuu Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Ester Mayala, Elizabeth Wambui, Precious Jentrix na Vivian Corazone na kuwaingiza Mary Saiki, Amina Bilal, Ritticia Nabbosa, Shelda Boniface na Mwanahamisi Omary.

Queens imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha pointi 25 kufuatia kucheza mechi tisa.

Back to homepage
Share this story