Simba Sports Club
News

Simba Queens yaichapa Fountain Gate Chamazi

10 Jun 2024

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini Jentrix Shikangwa alitupatia bao kwanza dakika ya 17.

Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya mashambulizi huku Fountain Gate nao wakijibu mashambulizi na kutawala mchezo katika eneo la katikati.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Aisha Mnuka dakika ya 60 kwa shuti kali baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Fountain Gate.

Advertisement

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 17 huku tukisalia na mchezo mmoja kabla ya kumaliza msimu.

Kocha Mussa Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Vivian Corazone, Daniela Ngoyi, Jentrix Shikangwa, Caroline Rufa na

Fatuma Issa na Danai Bhobho, Esther Mayalla, Janet Shija, Mwanahamis Omary na Silvia Thomas.

Back to homepage
Share this story