Simba Sports Club
News

Simba Queens Mabingwa TWPL 2023/24

7 Jun 2024

Ushindi huo unatufanya kufikisha pointi 46 ambazo haiwezi kufikiwa na timu yoyote huku tukiwa na tumebakiwa na michezo miwili.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao kwanza kwa kichwa dakika ya pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Wambui.

Ritticia Nabbosa alitupatia bao la pili dakika ya 20 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Alliance na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango.

Advertisement

Jentrix aliongeza bao la tatu dakika ya 40 na kukamilisha ushindi uliotupatia ubingwa ambao tuliupoteza msimu uliopita.

Kocha Mussa Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Zubega Mgunda, Esther Mayala, Zainabu Mohamed na Diana Mnally na kuwatoa Caroline Rufa, Daniela Ngoyi, Jentrix Shikangwa na Doto Evarist.

Back to homepage
Share this story