Queens itaondoka na kikosi cha wachezaji 25 tuliowasajili kwa ajili ya msimu huu ambao tunaamini watatufikisha kwenye malengo tuliyojiwekea.
Queens itaanza kutimua vumbi Agosti 18 kwa kucheza AFad Djibouti kutoka Djibouti mtanange utakaopigwa Uwanja wa Abebe Bikila.
Advertisement
Mchezo wa pili wa Queens utakuwa dhidi ya Kawempe Muslim utakaopigwa Agosti 20 katika Uwanja huo huo wa Abebe Bikila.
Simba Queens itakamilisha mchezo wa hatua ya makundi kwa kucheza dhidi ya RVP Buyenzi Agosti 22 pia katika dimba la Abebe Bikila.