Winfrida Gerrard aliipatia JKT Queens bao dakika ya 32 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upende wa kushoto na Stumai Abdallah.
Kipindi cha pili Simba Queens ilirudi kwa kasi na kifika zaidi langoni mwa JKT katika dakika 10 za mwanzo lakini walinzi wake walikuwa imara.
Zawadi Usanase alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 53 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja nje ya 18 baada ya Jentrix Shikangwa kufanyiwa madhambi.
Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya mashambulizi na kuliandama lango la JKT lakini tukikosa umakini wa kutumia nafasi tulizopata.
Kocha Mkuu, Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kumtoa Zawadi Usanase na kumuingiza Elizabeth Joseph dakika ya 58.
Matokeo haya yanaifanya Simba Queens kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa WPL baada ya kufikisha alama 19 kufuatia kushinda mechi sita na kutoka sare moja.