Mgosi amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu.
Mgosi amesema JKT ni timu nzuri na ipo kwenye kiwango bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua taji.
"Msimu uliopita tulishindwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii lakini safari hii tumejipanga. Upinzani ni mkubwa lakini tumejiandaa kwa ajili ya mchezo wa kesho," amesema Mgosi.
Nae nahodha wa timu, Esther Mayala amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kuhakikisha wanapambana ili kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii.
"Ni jambo la wazi kuwa tunahitaji ushindi kwenye mchezo wa kesho ingawa haitakuwa mechi rahisi. Tunajua mpira ni mchezo wa makosa lakini tumejiandaa na tupo tayari kwa ajili ya kupambana ili kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii," amesema Esther.