Simba Sports Club
News

Simba Queens ipo Kamili kuivaa Fountain Gate Kesho

16 Dec 2025

Mgosi amesema kikosi kimefanya mazoezi jana na leo pia kitafanya mara ya mwisho na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri kwa ajili ya kuipambania timu kupata alama tatu.

Mgosi ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na timu zote kuundwa na wachezaji wazoefu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda kama ilivyokuwa msimu uliopita.

"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunafahamu utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote lakini tumejipanga na tupo tayari kupambana mpaka mwisho," amesema Mgosi.

Advertisement

Kuhusu hali ya majeruhi kikosini kocha Mgosi amesema "ni kweli kuna wachezaji ambao tumewaacha Dar es Salaam kwa sababu ya majeruhi lakini hiyo haitufanyi kushindwa kupata ushindi, tuna kikosi kipana kucheza mechi yoyote."

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, mshambuliaji Aisha Mnunka amesema wamepata maandalizi mazuri na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho.

"Kila mchezaji yupo tayari, tunafahamu itakuwa mechi ngumu kwakuwa tunacheza ugenini lakini tumejipanga na tunaamini tutapata matokeo chanya kikubwa mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kutupa sapoti," amesema Mnunka.

Back to homepage
Share this story