Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na kiungo mshambuliaji, Zawadi Usanase kipindi cha kwanza baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Ruangwa.
Baada ya bao hilo tuliendelea kulisakama lango la Ruangwa na kutengeneza nafasi za kufunga ingawa tulishindwa kuzitumia ipasavyo.
Kwa nyakati tofauti kipindi cha pili Ruangwa nao walifanya mashambulizi kadhaa langoni kwetu lakini safi yetu ya ulinzi ilikuwa imara kuondoa hatari zote.
Advertisement
Kocha Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ambapo alimtoa Zawadi Usanase na kumuingiza Elizabeth Joseph dakika ya 75.
Ushindi huu unaifanya Simba Queens kufikisha alama 18 baada ya kucheza mechi sita na kushinda zote.