Simba Sports Club
News

Simba, Mlandege Hakuna Mbabe

7 Jan 2022

Licha ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Mlandege tumefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar.

Matokeo haya yametufanya kufikisha alama nne na kuwa kinara wa kundi C.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku mashambulizi yakiwa machache kutoka kwa timu zote.

Advertisement

Kipindi cha pili kasi iliongezeka kiasi huku tukipoteza nafasi mbili za wazi ambazo zingetufanya kupata mabao.

Kocha Pablo Franco aliwaingizaDavid Udoh, Cheick Mukoro, Bernard Morrison, Shomari Kapombe na Medie Kagere na kuwatoa Yussuf Mhilu, Chris Mugalu, Pape Sakho, Kibu Denis na Gadiel Michael.

Back to homepage
Share this story