Baada ya ushindi wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza leo, kikosi chetu kitarejea jijini Dar es Salaam usiku.
Kikosi kitakapotua jijini wachezaji watapewa mapumziko ya siku chache kuonana na familia zao kabla ya kurejea mazoezini.
Advertisement
Baada ya mapumziko hayo kikosi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 28, mwaka huu.