Kikosi chetu kitaondoka Ijumaa kuelekea nchini Botswana kwa mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Jwaneng Galaxy.
Kikosi kitaondoka na wachezaji wote walio fiti na kamili kwa ajili ya mchezo huo ambao tunahitaji kufanya vizuri ili mechi ya marudiano nyumbani iwe rahisi.
Advertisement
Mchezo wetu dhidi ya Jwaneng utapigwa Jumapili Oktoba, 17 wakati marudiano yatakuwa Oktoba, 24 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.