Simba Sports Club
News

Simba kuondoka asubuhi kuifuata Red Arrows

2 Dec 2021

Kikosi chetu kitaondoka kesho asubuhi kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mechi yetu ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows itakayopigwa Jumapili Desemba 5.

Kikosi kitaondoka kikiwa na wachezaji 25 tayari kwa mchezo huo ambao tutaingia tukiwa na mtaji wa mabao 3-0.

Advertisement

Kaimu Msemaji wa klabu, Ally Shatry (Chico) amesema maandalizi ya safari yamekamilika na kila kitu kimekaa kwenye nafasi yake.

Back to homepage
Share this story