Mchezo wetu wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Botswana utapigwa Oktoba 17 katika Uwanja wa Taifa wa Botswana saa 10 jioni kwa saa za nyumbani.
Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa kati ya Oktoba 14 na 15 nchini Botswana lakini leo tumepokea taarifa rasmi kuwa utapigwa Oktoba 17.
Advertisement
Aidha, mchezo wa marudiano utapigwa Oktoba 24 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.