Simba Sports Club
News

Simba hakuna kulala, yafanya mazoezi muda mfupi baada ya kutua

3 Dec 2021

Baada ya kutua nchini Zambia jioni kikosi kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili licha ya kuchelewa kufika kama ilivyotarajiwa.

Awali ilikuwa tufike Zambia saa saba mchana lakini kutokana na taratibu za usafiri kuchelewa ikabidi tufike jioni na kikosi kikaenda moja kwa moja mazoezini.

Advertisement

Kocha Mkuu Pablo Franco ametaka wachezaji kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili ili kuondoa uchovu wa safari.

Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuwavaa Red Arrows Jumapili saa 10 jioni kwa saa za nyumbani.

Back to homepage
Share this story