Kabla ya kilele cha Simba Day kutatanguliwa na wiki ya Simba itakayoanza Agosti Mosi ambapo wanachama, mashabiki na wapenzi wetu nchi nzima watafanya shughuli za kijamii.
Shughuli hizo za kijamii ni kama kutoa misaada kwa wenye uhitaji kama vituo vya watoto yatima, wazee, magereza, hospitali na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali kama shuleni na mengineyo.
Siku ya kilele cha Simba Day huwa tunaitumia kutambulisha kikosi chetu pamoja na jezi tutakazotumia kwa ajili msimu ujao wa ligi.
Kabla ya Simba Day tutazindua kwanza jezi zetu ili kuwapa nafasi mashabiki kununua ili kupendezesha uwanja siku ya tukio hilo kubwa linalosubiriwa kwa hamu.
Kuhusu timu ambayo tutacheza nayo siku hiyo utaratibu unaendelea kufanywa na mara utakapokamilika tutaitangaza rasmi kwa wanachama na mashabiki wetu.