Shikangwa alifunga mabao hayo yote kipindi cha pili kufuatia kwenda mapumziko timu zikiwa hazijafungana licha ya kushambuliana kwa zamu.
Hat trick hiyo ya kwanza kwa Shikangwa imemfanya mshambuliaji huyo raia wa Kenya kuanza kukaa kileleni kwenye orodha ya ufungaji ya TWPL mpaka sasa.
Ikumbukwe msimu uliopita, Shikangwa alimaliza akiwa nafasi ya pili kwa kufumania nyavu ambapo sasa amerejea na kasi ile ile aliyokuwanayo msimu wa 2024/2025.
Advertisement
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia kutokana na timu zote kuonyesha kandanda safi bao jingine lilifungwa na mshambuliaji, Aisha Mnunka.
Kocha Mussa Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Zawadi Usanase, Dotto Evarist na Zanga Brice na kuwaingiza Vivian Corazone, Elizabeth Wambui na Asha Omary.