Shikangwa raia wa Kenya ameendeleza moto wake wa kucheka na nyavu ambapo katika mechi mbili zilizopita amefunga mabao saba kufuatia wiki iliyopita kufunga manne dhidi ya Mlandizi Queens.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali muda wote bao letu jingine lilifungwa na kiungo mkabaji Vivian Corazone.
Mabao ya Fountain Gate yaliwekwa kambani na Amina Hemed pamoja na Maria Elia.
Advertisement
Kocha Mkuu Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Asha Djafar, Aisha Mnuka, Violeth Nicholas, Precious Christopher na Esther Mayala na kuwaingiza Elizabeth Wambui, Ritticia Nabbosa, Janeth Nyagali, Emiliana Mdimu na Shelda Boniface.
Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 31 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 11.