Nyota wetu wa zamani, Sharaf Eldin Shiboub na winga Moukoro Cheik Tenena kutoka Ivory Coast wataanza majaribio katika Michuano ya Mapinduzi na kama wakiweza kulishawishi benchi la ufundi watasajiliwa katika dirisha hili dogo.
Shiboub alikuwa nasi miaka miwili iliyopita na amerejea tena lakini safari hii ataanza majaribio kabla ya kujiunga kama atafanya vizuri.
Advertisement
Kwa upande wake Tenena ambaye amewahi kuzichezea timu mbalimbali ndani ya Afrika kama Al Masry ya Misri na Al Hilal ya Sudan naye amekuja kujaribu bahati yake.
Tayari nyota hao wako Visiwani Zanzibar pamoja na kikosi kwa michuano hiyo ambapo tutaanza kutupa karata yetu ya kwanza Jumatano.