Ahmed ameyasema hayo akiwa Tawi la Tabata Old Dampo ikiwa ni siku ya pili ya zoezi la hamasa kuelekea mchezo huo ambao lengo letu ni moja kuitoa Al Masry na kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Ahmed amesema lengo la kumualika Sheikh Walid mbali na kuja kushuhudia kandanda safi lakini pia kufanya Dua kama kuna wenye husuda washindwe ili kuiwezesha timu kutinga nusu fainali.
"Mchezo dhidi ya Al Masry ni muhimu kwetu na tunahitaji kushinda na kufuzu nusu fainali ndio maana tumejiandaa kwenye kila hali na pia tumejikabidhi kwa Mwenyezi Mungu ndio maana tumemualika Sheikh Walid Alhad Omar," amesema Ahmed.
Sheikh Walid anakuwa kiongozi wa pili wa dini kualikwa kwenye mchezo wetu dhidi ya Al Masry baada ya Mtumishi wa Mungu Mtume Boniface Mwamposa 'Buldozer' kutangazwa nae kuwa atakuwepo.