Mashabiki hao ambao asilimia kubwa wamekuja kuuza na kununua ng'ombe wamenogesha zoezi letu la hamasa kwa kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali za hamasa.
Kama kawaida zoezi la kuuza tiketi pamoja na jezi limekuwa na mapokeo mazuri kutokana na jinsi mashabiki walivyojitokeza.
Advertisement
Msafara wa zoezi la hamasa leo umeanzia Buguruni Sheli, tukapitia Mombasa Gongo la Mboto tukasimama kuhamasisha, tulipofika Gongo la Mboto tukasimama pia hadi tulipofika Pugu Mnadani.
Mapokezi tuliyopata Pugu Mnadani ni makubwa na inakuwa moja ya sehemu ambayo Wanasimba wamejitokeza kwa wingi katika maeneo tuliyopita kwenye zoezi hili la hamasa.