Simba Sports Club
News

Sakho: Tunaenda Guinea kupambana kupata Ushindi

9 Feb 2023 By simba 319 views
  Kiungo mshambuliaji, Pape Sakho ameweka wazi kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunashinda ugenini dhidi ya Horoya katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigiwa Jumamosi. Sakho amesema kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo huo na yupo tayari kuhakikisha anapigania timu kupata matokeo mazuri ugenini. Akizungumzia kukosekana kwa kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza amesema alitamani angekuwepo kikosini kutokana na ubora na uzoefu wake lakini siku zote majeruhi sio kitu kizuri kwa mchezaji. "Maandalizi yetu ni mazuri, malengo yetu ni kushinda ugenini tutapambana ili kufanikisha hilo. "Tunajua haitakuwa mechi rahisi, tutakuwa ugenini lakini tupo tayari kwa mpambano na mashabiki wetu tunawaomba mtuombee ili tukatimize malengo," amesema Sakho.
Advertisement
Back to homepage
Share this story