Simba Sports Club
News

Sakho, Kanoute wako fiti

14 Feb 2022

Nyota wetu Pape Sakho na Sadio Kanoute ambao walishindwa kuendelea na mchezo wa jana wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas wamefanyiwa uchunguzi na daktari na kubainika wako fiti.

Baada ya uchunguzi huo wa daktari wawili hao wamepewa mapumziko ya siku moja kabla ya kesho kurudi mazoezini kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Jumatano.

Advertisement

Awali ilionekana huenda nyota hao wamepata majeraha makubwa lakini baada ya uchunguzi imeonekana ni maumivu madogo ambapo wanaweza kumudu kushuka uwanjani Jumatano.

Back to homepage
Share this story