Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amesema hana hofu na mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas kwa kuwa tuna kikosi ambacho kinaweza kushinda katika uwanja wowote.
Sakho raia wa Senegal amekuwa gumzo barani Afrika kutokana na kiwango chake pamoja na kufunga mabao mawili ambayo yamechaguliwa magoli bora ya mashindano kwa nyakati tofauti.
Kuhusu kutinga robo fainali Sakho amesema bila shaka tutatinga kwa sababu tumekuja Benin tukiwa na lengo la kupambana kuchukua alama tatu na kurudi nazo jijini Dar es Salaam.
"Simba ni timu kubwa na ina kikosi bora, tunaweza kupata alama tatu katika uwanja wowote ndani ya Afrika. Tunajua ASEC ni timu nzuri lakini tumejipanga na lengo letu ni kuhakikisha tunachukua alama zote tatu," amesema Sakho.
Kuhusu kufunga magoli bora ya mashindano Sakho amesema ataendelea kufanya hivyo kila atakapopata nafasi kwani lengo lake ni kuisaidia timu kushinda kila mchezo.