Sakho alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata maumivu wakati Baleke alitolewa uwanjani kwa msaada machela hali iliyozua taharuki miongoni mwa mashabiki wa Simba.
Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema nyota hao hawakupata madhara makubwa hivyo wanaendelea vema na kesho wataendelea na programu ya mazoezi kama kawaida.
"Sakho na Baleke walipata maumivu katika mchezo wa jana lakini hawakupata madhara makubwa hivyo wanaendelea vizuri na kesho wataendelea na programu za mazoezi," amesema Dk. Edwin.
Kuhusu Augustine Okrah ambae nae alishindwa kuendelea na mchezo Dk. Kagabo amesema wanasubiri majibu ya vipimo vya CT Scan ili kupata uhakika wa majeraha aliyopata nyota huyo.
"Uwezakano wa Okrah kuanza mazoezi hivi karibuni ni mdogo kwa sababu bado anasikia maumivu ya mguu, tunasubiri vipimo vya CT Scan ili kujua ukubwa wa jeraha lake," amesema Dk. Edwin.
Wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja baada ya kumaliza mchezo wa jana watarejea mazoezini kesho kuanza maandalizi ya mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya itakayopigwa Februari 11 nchini Guinea.