Simba Sports Club
News

Sakho aumia mazoezini

29 Mar 2022

Sakho alishindwa kuendelea na mazoezi hayo ambapo mara moja alianza kupatiwa matibabu na sasa hali yake inaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa daktari jeraha la Sakho si kubwa hivyo amepatiwa matibabu ambapo leo amepewa mapumziko na atarejea mazoezini kesho Jumatano.

Advertisement

Madaktari wamewatoa hofu Wanasimba kuwa nyota huyo anaendelea vema na kesho atarejea mazoezini na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani Jumapili kuikabili US Gandermarie.

Kwa sasa wachezaji wote wapo katika hali nzuri kiafya isipokuwa Hassan Dilunga ambaye bado anaendelea kupata matibabu

Back to homepage
Share this story