Simba Sports Club
News

Sakho aridhia kumwachia Chama namba 17

16 Jan 2022 By simbasc 3,148 views

Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amekubali kumwachia jezi namba 17 Clatous Chama ambayo alikuwa anaitumia tangu ajiunge nasi katika majira ya kiangazi yaliyopita.

Kabla ya kuondoka na kujiunga na RS Berkane, Chama alikuwa anavaa jezi namba 17 ambayo ndiyo inamtambulisha.

Sakho sasa atavaa jezi namba 10 ambayo imeachwa na Ibrahim Ajibu aliyejiunga na Azam FC.

Advertisement

Baada ya kumkabidhi Chama jezi hiyo, Sakho amesema amefanya hivyo kwa heshima ya fundi huyo kutokana na makubwa aliyofanya ndani ya timu.

"Nimekubali kumwachia namba 17 Chama kutokana na heshima niliyo nayo kwake, amefanya makubwa ndani ya timu. Nitatumia jezi namba 10 kuanzia sasa," amesema Sakho.

Back to homepage
Share this story